Kila mwaka, mamilioni ya watu wanaoishi Marekani wanafanya Tax Return zao kwa serikali ya Marekani kupitia shirika linaloitwa Internal Revenue Service (IRS). Watu wengine wanafanya Tax Return ili warudishiwe pesa zao, ambazo zinaitwa Tax Refund, na wengine wanafanya Tax Return ili kulipa kodi wanazodaiwa na serikali.

Lakini wakati watu wengi wanafanya Tax Return zao, kuko pia watu wabaya ambao wanajaribu kutumia taarifa za watu wengine ili kuiba pesa za Tax Refund. Watu hawa wanaweza kutumia Social Security Number (SSN) ya mutu mwingine na kufanya Tax Return kwa jina lake bila ruhusa yake.

Kulingana na taarifa za IRS, katika mwaka wa 2025, kulikuwa na karibu Tax Returns milioni 165.8 zilizopokelewa na IRS. Kati ya hizo, karibu milioni 154.9 zilifanywa kwa njia ya internet, ambayo inaitwa Electronic Filing (IRS, 2025).

Hii inaonyesha namna watu wengi wanatumia internet kufanya Tax Return zao. Lakini pia inaonyesha umuhimu wa kila mutu kulinda taarifa zake za kibinafsi.

Kwa kusaidia watu kujilinda na wizi wa taarifa zao, IRS ilianzisha program inayoitwa Identity Protection Personal Identification Number (IP PIN).

Program hii ni ya bure kabisa na inaweza kusaidia kuzuia mutu mwingine kufanya Tax Return kwa kutumia Social Security Number yako bila ruhusa yako.

Lakini IP PIN ni nini hasa? Ni nani anaweza kuipata? Na namna gani unaweza kujiandikisha ili upate IP PIN yako?

Katika makala hii, tutaeleza mambo hayo kwa lugha rahisi ili kila mutu aweze kuelewa.

Kumbuka

IP PIN ni bure, ina tarakimu sita, na inabadilika kila mwaka. Tumia IP PIN ya mwaka ambao unatuma Tax Return yako.

IP PIN ni Nini?

Identity Protection Personal Identification Number, ambayo inajulikana kwa jina la IP PIN, ni namba ya siri yenye tarakimu sita (6) ambayo IRS inapatia watu ili kusaidia kulinda taarifa zao wakati wanafanya Tax Return.

Namba hii inasaidia IRS kuhakikisha kwamba Tax Return inayofanywa kwa jina lako inatoka kwako, na si kwa mutu mwingine anayetumia taarifa zako bila ruhusa.

Kwa mfano, fikiria mutu fulani ameiba Social Security Number yako. Mutu huyo anaweza kujaribu kufanya Tax Return kwa jina lako ili achukue Tax Refund yako.

Lakini kama uko na IP PIN, itakuwa vigumu kwake kufanya hivyo kwa sababu IRS itahitaji pia ile namba yako ya siri yenye tarakimu sita.

Bila IP PIN sahihi, Tax Return anayojaribu kutuma kwa njia ya Electronic Filing itakataliwa na IRS.

IP PIN haibadilishi Social Security Number yako. Ni namba ya ziada inayosaidia kulinda taarifa zako.

Jambo lingine la muhimu ni kwamba IRS inabadilisha IP PIN kila mwaka. Hii inamaanisha kwamba IP PIN ya mwaka wa 2026 haiwezi kutumiwa kufanya Tax Return katika mwaka wa 2027.

Kulingana na IRS (2026), lengo kubwa la program hii ni kusaidia kuzuia watu wabaya kutumia Social Security Number au ITIN za watu wengine kufanya Tax Return za uongo.

Ni Nani Anaweza Kupata IP PIN?

Watu wengi wanafikiri kwamba IP PIN inapewa tu watu ambao tayari wameibiwa taarifa zao.

Lakini hiyo si kweli.

IRS inaruhusu watu wanaotimiza masharti kujiandikisha na kupata IP PIN, hata kama hawajawahi kuibiwa taarifa zao.

Ili uweze kupata IP PIN, unahitaji kuwa na Social Security Number (SSN) au Individual Taxpayer Identification Number (ITIN), na uweze kuthibitisha kwamba wewe ni mutu unayesema kuwa.

Hii inamaanisha kwamba raia wa Marekani (U.S. Citizens), watu wenye Green Card, na watu wanaotumia ITIN wanaweza kuomba IP PIN.

Hata watu ambao wanaishi nje ya Marekani wanaweza kupata IP PIN kama wanatimiza masharti ya IRS.

Watu waliooana wanaweza pia kupata IP PIN zao, na watoto wanaweza kupewa IP PIN kupitia utaratibu unaokubaliwa na IRS.

Jambo la kufurahisha ni kwamba hauhitaji kuwa na mapato mengi ili kupata IP PIN. Pia hauhitaji kulipa pesa yoyote.

Program ya IP PIN ni bure kabisa.

Kwa hiyo, kama uko na SSN au ITIN na unaweza kuthibitisha utambulisho wako, unaweza kujiandikisha.

Kwa Nini IP PIN ni ya Muhimu?

Wizi wa taarifa za watu, ambao kwa English unaitwa Identity Theft, unaweza kuleta matatizo makubwa, hasa wakati wa kufanya Tax Return.

Fikiria kwamba unategemea Tax Refund yako ili ulipe nyumba, ununue chakula, ulipe bills, au usaidie familia yako.

Lakini wakati unajaribu kufanya Tax Return, unagundua kwamba mutu mwingine tayari alifanya Tax Return kwa kutumia Social Security Number yako.

Hali kama hii inaweza kufanya IRS isimamishe Tax Return yako kwa muda wakati inachunguza tatizo hilo.

Kulingana na National Taxpayer Advocate’s 2025 Annual Report to Congress, iliyotolewa mwezi wa January 2026, mamia ya maelfu ya watu waliokuwa na matatizo ya Identity Theft walikuwa wakisubiri kwa muda mrefu ili matatizo yao yatatuliwe.

Ripoti hiyo ilionyesha kwamba kesi za Identity Theft Victim Assistance zilikuwa zinachukua kwa wastani zaidi ya miezi 21 kutatuliwa.

Fikiria kusubiri karibu miaka miwili ili tatizo la Tax Return yako litatuliwe na upate Refund yako!

Kwa mutu ambaye alikuwa anategemea pesa hizo ili kusaidia familia yake, kusubiri muda mrefu namna hiyo kunaweza kuleta matatizo makubwa ya kifedha.

Ndiyo sababu ni vizuri kujilinda mbele ya wakati.

IP PIN haiwezi kuzuia kila aina ya wizi wa taarifa zako, lakini inaweza kusaidia sana kuzuia mutu mwingine kufanya Electronic Tax Return kwa kutumia taarifa zako bila ruhusa.

Na jambo la muhimu zaidi ni kwamba hauhitaji kulipa kampuni fulani ili upate ulinzi huu.

IRS inakupatia IP PIN bure.

Namna Gani Unaweza Kujiandikisha na Kupata IP PIN?

Njia rahisi na ya haraka ya kupata IP PIN ni kupitia website rasmi ya IRS.

Kwanza, fungua website ya IRS kupitia link hii: IRS.gov/IPPIN.

Ukiingia kwenye website hiyo, utaona maelezo kuhusu IP PIN na namna ya kujiandikisha.

Kama tayari uko na IRS Online Account, unaweza kuingia kwenye account yako.

Lakini kama hauna IRS Online Account, utahitaji kufungua account mpya.

IRS inatumia huduma inayoitwa ID.me ili kusaidia kuthibitisha utambulisho wa watu wanaotumia huduma zake za internet.

Wakati wa kufungua account, unaweza kuombwa utoe taarifa zako za kibinafsi na documents zinazohitajika ili kuthibitisha kwamba account ni yako.

Baada ya kuingia kwenye IRS Online Account yako, utaenda kwenye sehemu inayoitwa Profile.

Katika sehemu hiyo, utapata nafasi ya kujiandikisha kwenye program ya Identity Protection PIN.

IRS inatoa njia mbili za kujiandikisha.

Njia ya kwanza inaitwa Continuous Enrollment. Ukichagua njia hii, utaendelea kuwa kwenye program ya IP PIN kila mwaka. IRS itakuwa inakupatia IP PIN mpya kila mwaka.

Njia ya pili inaitwa One-Time Enrollment. Ukichagua njia hii, utapewa IP PIN ya mwaka huo tu. Mwaka ukiisha, hautaendelea moja kwa moja kwenye program hiyo.

Baada ya kumaliza kujiandikisha, utaweza kuona IP PIN yako yenye tarakimu sita kwenye IRS Online Account yako.

Ni vizuri kuweka namba hiyo mahali salama kwa sababu utaihitaji wakati wa kufanya Tax Return yako.

Get Your IRS IP PIN ↗

Kama Hauwezi Kujiandikisha Kupitia Internet, Utafanya Nini?

Si kila mutu anaweza kufungua IRS Online Account bila matatizo.

Watu wengine wanaweza kushindwa kuthibitisha utambulisho wao kupitia ID.me, na wengine wanaweza kuwa na matatizo ya kutumia internet.

Kwa sababu hiyo, IRS imeweka njia zingine za kupata IP PIN.

Njia moja ni kutumia IRS Form 15227, ambayo jina lake kamili ni Application for an Identity Protection Personal Identification Number.

Kulingana na Form 15227 ya January 2026, njia hii inaweza kutumiwa na watu wanaotimiza masharti na ambao Adjusted Gross Income yao kwenye Tax Return yao ya mwisho ilikuwa chini ya $84,000.

Kwa watu waliooana na wanaofanya Tax Return pamoja, yaani Married Filing Jointly, kiwango hicho ni chini ya $168,000.

Pia unahitaji kuwa na SSN au ITIN na namba ya simu ambayo IRS inaweza kutumia kukupigia ili kuthibitisha utambulisho wako.

Baada ya IRS kupokea application yako, inaweza kukupigia simu ili kuhakikisha kwamba wewe ndiye mutu aliyeomba IP PIN.

Njia nyingine ni kwenda kwenye ofisi ya IRS inayoitwa Taxpayer Assistance Center.

Unaweza kufanya appointment kwa kupiga simu kwenye namba: 844-545-5640.

Ukienda kwenye appointment yako, utahitaji kubeba documents zinazoweza kuthibitisha utambulisho wako.

Njia hizi zinaweza kuchukua muda mrefu zaidi kuliko kujiandikisha kupitia IRS Online Account.

IRS Form 15227 ↗ · 844-545-5640

Je, IP PIN Inabadilika Kila Mwaka?

Ndiyo.

IRS inatoa IP PIN mpya kila mwaka.

Kwa mfano, kama ulipata IP PIN katika mwaka wa 2026, utatumia namba hiyo wakati wa kufanya Tax Return zinazotumwa katika mwaka wa 2026.

Lakini ukifika mwaka wa 2027, utahitaji kutumia IP PIN mpya ya 2027.

Hata kama unafanya Tax Return ya mwaka uliopita, unatakiwa kutumia IP PIN ya mwaka ambao unatuma Tax Return hiyo.

Kwa watu waliojiandikisha kupitia IRS Online Account, IP PIN mpya inaweza kupatikana kwenye account yao kila mwaka.

Kama umesahau IP PIN yako, ni vizuri kuirudisha kupitia IRS Online Account kabla ya kutuma Tax Return yako.

Usijaribu kubahatisha namba hiyo.

Kama utaweka IP PIN isiyo sahihi, IRS inaweza kukataa Electronic Tax Return yako.

Na kama unatuma Tax Return kwa karatasi bila IP PIN inayohitajika, inaweza kuchukua muda mrefu zaidi kushughulikiwa.

Je, Bibi Yako, Bwana Yako, au Watoto Wako Wanaweza Kupata IP PIN?

Ndiyo.

IRS inaruhusu watu waliooana na watoto wanaotimiza masharti kupata IP PIN zao wenyewe.

Kwa mfano, kama wewe na bibi yako mnafanya Tax Return pamoja, kila mmoja wenu anaweza kuwa na IP PIN yake.

Kama nyote wawili muko na IP PIN, namba za kila mmoja zinapaswa kuwekwa kwenye Tax Return yenu.

Watoto pia wanaweza kupata IP PIN.

Hili ni jambo la muhimu kwa sababu hata Social Security Number ya mutoto inaweza kutumiwa vibaya na watu wengine.

Wazazi au walezi wanaweza kuomba IP PIN kwa ajili ya watoto wao kupitia njia zinazokubaliwa na IRS.

Kwa watoto walio chini ya miaka 18, maombi yanafanywa kupitia njia mbadala, kama Form 15227 au appointment kwenye IRS Taxpayer Assistance Center.

Kulinda taarifa za watoto ni jambo la muhimu kwa sababu matatizo ya Identity Theft yanaweza kugunduliwa baada ya muda mrefu.

Je, Unaweza Kupatia Tax Preparer Wako IP PIN Yako?

IP PIN ni namba ya siri ambayo unapaswa kuilinda vizuri.

Lakini kama unatumia Tax Preparer ambaye unamuamini ili akusaidie kufanya Tax Return yako, utahitaji kumpatia IP PIN yako wakati uko tayari kusaini na kutuma Tax Return.

Hii ni kwa sababu Tax Preparer atahitaji kuweka namba hiyo kwenye Tax Return yako.

Hata hivyo, usipatie IP PIN yako kila mutu.

IRS inashauri watu kushiriki IP PIN zao tu na Tax Preparer wanayemuamini wakati wa kufanya Tax Return.

Pia, IRS haitakupigia simu, kukutumia email, au text message ili kukuomba IP PIN yako.

Kwa hiyo, kama unapokea message kutoka kwa mutu anayesema anatoka IRS na anakuomba IP PIN yako, kuwa mwangalifu.

Inaweza kuwa ni scam.

Je, Ukiwa na IP PIN Utapata Tax Refund Yako Haraka Zaidi?

Hapana.

IP PIN haikutengenezwa ili kufanya Tax Refund yako itoke haraka.

Lengo lake kubwa ni kulinda taarifa zako na kusaidia kuzuia watu wengine kufanya Tax Return kwa jina lako bila ruhusa.

Hata kama uko na IP PIN, IRS inaweza kuchunguza Tax Return yako kama kuna taarifa ambazo zinahitaji kuthibitishwa.

Kwa hiyo, kuwa na IP PIN haimaanishi kwamba Refund yako itatoka haraka kuliko ya watu wengine.

Lakini inaweza kukusaidia kupunguza hatari ya mutu mwingine kutumia taarifa zako kufanya Tax Return ya uongo.

Je, Kila Mutu Analazimishwa Kuwa na IP PIN?

Hapana.

Kwa watu wengi, kujiandikisha kwenye program ya IP PIN ni jambo la kuchagua.

Lakini kama IRS tayari ilikupatia IP PIN, utahitaji kuitumia wakati wa kufanya Tax Return zinazohitaji namba hiyo.

Watu wengine ambao walijiandikisha kwa kupenda kwao wanaweza kuwa na nafasi ya kujiondoa kwenye program hiyo.

Lakini watu ambao IRS iliwaingiza kwenye program kwa sababu walikuwa victims wa Identity Theft wanaweza kuwa na masharti tofauti.

Ndiyo sababu ni vizuri kuelewa namna program inafanya kazi kabla ya kujiandikisha.

Hitimisho: Linda Taarifa Zako Kabla Matatizo Hayajatokea

Wizi wa taarifa za watu ni tatizo kubwa ambalo linaweza kuleta shida nyingi, hasa wakati wa kufanya Tax Return.

Watu wengine wanaweza kupoteza muda mwingi wakijaribu kuthibitisha kwa IRS kwamba wao ndio wenye Social Security Number iliyotumiwa kufanya Tax Return ya uongo.

Wengine wanaweza kusubiri miezi mingi kabla ya kupata Tax Refund zao.

Kama tulivyoona kwenye ripoti ya National Taxpayer Advocate, matatizo ya Identity Theft yanaweza kuchukua muda mrefu kutatuliwa.

Lakini habari nzuri ni kwamba IRS imeweka program ya bure ambayo inaweza kusaidia watu kujilinda.

Program hiyo ni Identity Protection PIN (IP PIN).

Kama uko na Social Security Number au ITIN na unaweza kuthibitisha utambulisho wako, ni vizuri kufikiria kujiandikisha kwenye program hii.

Hauhitaji kusubiri mpaka mutu aibe taarifa zako ndipo uanze kujilinda.

Ni vizuri kujilinda leo kuliko kungoja matatizo yakupate kesho.

Kwa kupata maelezo zaidi au kuomba IP PIN yako, tembelea website rasmi ya IRS.

Get Your IRS IP PIN ↗

References

  1. Internal Revenue Service. (2025). Filing season statistics for week ending December 26, 2025.

    IRS Filing Season Statistics ↗
  2. Internal Revenue Service. (2026). Frequently asked questions about the identity protection personal identification number (IP PIN).

    IRS IP PIN Frequently Asked Questions ↗
  3. Internal Revenue Service. (2026). Form 15227: Application for an Identity Protection Personal Identification Number.

    IRS Form 15227 ↗
  4. National Taxpayer Advocate. (2026). 2025 Annual Report to Congress. Taxpayer Advocate Service.

    National Taxpayer Advocate Annual Report ↗
  5. Internal Revenue Service. (2026). Get an identity protection PIN.

    Get Your IRS IP PIN ↗

Disclaimer: Makala hii imeandikwa kwa ajili ya kutoa elimu na taarifa kwa wasomaji. Si ushauri wa Tax au sheria kwa hali ya kila mutu. Sheria na taratibu za IRS zinaweza kubadilika. Kwa maelezo yanayohusu hali yako binafsi, ni vizuri kusoma taarifa rasmi za IRS au kuzungumza na Tax Professional mwenye ujuzi.

© 2026 Faraja Mbindula. All Rights Reserved.

← Makala zote / All articles